Jeshi la Polisi nchini limesema kuwa litahakikisha linawakamata wahusika wote wa mauaji yaliyotokea katika Wilaya za Kibiti, Mkuranga na Rufiji mkoa wa Pwani ili kuwahakikishia usalama wananchi wanaoishi maeneo hayo.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, Inspekta Jenerali Simon Sirro alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, amesema kuwa pamoja na nchi kuwa shwari kwa sasa lakini jeshi la polisi bado linaendelea na operesheni mbalimbali nchini ili kuweza kuwabaini watu wanaojihusisha na uhalifu.

“Kipaumbele chetu cha kwanza ni kuhakikisha wanapatikana wale wote waliohusika na mauaji ya kule Kibiti, Mkuranga na Pwani, kwani hakuna mtu anayeweza kujichukulia sheria mikononi,”amesema Sirro.

Hata hivyo, Sirro amewataka bodaboda kutii sheria za usalama barabarani na kuacha kujihusisha na vitendo vya uhalifu pia amewaasa wananchi kuacha tabia ya kujichukulia sheria mikononi wanapo wakamata wahalifu.

Zambia Kucheza Robo Fainali Kombe La Dunia
Serikali yatangaza mikakati mipya vita ya dawa za kulevya