Mabingwa wa Afrika chini ya umri wa miaka 20, timu ya taifa ya Zambia wamefanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ya michuano ya kombe la dunia chini ya umri wa miaka 20, inayoendelea Korea Skuini.

Zambia wametinga robo fainali baada ya kuichabanga Ujerumani mabao manne kwa matatu. Hata hivyo haikua kazi rahisi kwa mabingwa hao wa Afrika kupata ushindi huo, kwani iliwalazimu kusubiri hadi dakika 30 za nyongeza, baada ya kumaliza dakika 90 wakiwa sawa na wapinzani wao kutoka Ulaya kwa kufungana mabao matatu kwa matatu.

Zambia walikua wakiongoza kwa mabao matatu kwa moja mpaka dakika ya 89, lakini umahiri wa kikosi cha Ujerumani kupitia kwa Suat Serdar na Jonas Arweiler ulifanikisha timu hizo kutoshanga nguvu.

Katika dakika 30 za nyongeza, Zambia walipata bao la ushindi dakika ya 107 kuputia kwa Shemmy Mayembe, ambaye alionekana kama okombozi wa taifa hilo la kusini mwa Afrika.

Bao la kwanza la Ujerumani lilifungwa na Philipp Ochs dakika ya nane, lakini Emmanuel Banda, Fashion Sakala na Enock Mwepu waliifungia Zambia mabao matatu.

Zambia itacheza na mshindi kati ya Italia na Ufaransa katika hatua ya robo fainali siku jumatatu.

Saad Kawemba: Nitaondoka Azam FC Kwa Utaratibu
Video: Sirro atangaza operesheni kali mkoa wa Pwani