Bosi wa CMB, Birdman ametangaza nia ya kumtajirisha mara mbili rapa 50 Cent kwa kusimamia uandaaji na usambazaji wa albam ijayo ya kiongozi huyo wa G-Unit.

Birdman ametumia mtandao wa Instagram kueleza kuwa ameshafanya mazungumzo na 50 akimtaka kumruhusu kuandaa albam hiyo itakayobatizwa jina la ‘Get Rich or Die Trying Part 2’, ikiwa ni muendelezo wa jina la albam iliyowahi kuweka rekodi kubwa zaidi ya mauzo kwa rapa huyo.

“Nimemwambia 50 Cent nataka kusimamia utayarishaji wa albam yake ijayo, ina uhakika wa kuvuka mauzo ya platinum #getrixhordietrying. P2,” tafsiri isiyo rasmi ya alichokiandika Birdman.

Get Rich Or Die Trying ilifanikiwa kufikia viwango vya platinum ikiuza nakala 872,000 ndani ya wiki moja, huku ikishikilia nafasi ya kwanza kwenye Billboard’s 200 Chart.

Hivi karibuni, iliripotiwa kuwa Birdman ameliweka sokoni jumba lake la kifahari lenye thamani ya zaidi ya dola za kimarekani milioni 20. Huenda fedha hizo zikawa zinampa kiburi cha kuwekeza kwenye kitu kizito kwa faida mara mbili.

Mr Blue aeleza wasiwasi wake juu ya muziki wa Bongo Fleva
Ederson Santana de Moraes Atua Etihad Stadium