Chama cha Mapinduzi (CCM) kimetoa pongezi za dhati kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa chama hicho kwa hatua yake ya uthubutu wa kusimamia raslimali za Taifa.
Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es salaam, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole amesema katika histori ya nchi, hatua zilizochukuliwa na Rais Magufuli hazijawahi kuonekana popote, hivyo inashangaza kuona baadhi ya wanasiasa wanakejeli hatua hizo za kishujaa zilizochukuliwa na Rais.
Amesema kilichofanywa na Rais Magufuli ni utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM ambayo imeelekeza kukomesha wizi unaofanywa na baadhi ya Wawekezaji katika Migodi ya Madini hapa nchini.
Polepole amesema viongozi waliotajwa katika taarifa mbili za uchunguzi wa Mchanga wa Madini wachukuliwe hatua stahiki kwani wamelisababishia taifa hasara kubwa ya Matrilioni ya Fedha, kutokana na Mchanga wa Madini kwenda nje ya nchi.
Aidha, amesisitiza kuwa CCM haitasita kuchukua hatua kwa wanachama wake iwapo watabainika kuliingizia Taifa hasara kupitia Mchanga wa Madini.
Pia, Polepole amepongeza hatua za awali zilizooneshwa na Mmliki wa Kampuni ya Barrick Gold Cooparation kwa kukiri kukosea na kuahaidi kufanya mazungumzo na Serikali ili kulipa fedha wanazodaiwa baada ya mazungumzo. Tazama hapa video