Beki kutoka nchini Mali Hamari Traore, amekamilisha safari ya kujiunga na klabu ya ligi daraja la kwanza Ufaransa (Ligue 1) Rennes, akitokea ligi daraja la pili alipokua akiitumikia Stade Reims.

Hamari amejiunga na Rennes kwa mkataba wa miaka minne ambao utafikia kikomo mwaka 2021.

Beki huyo mwenye umri wa miaka 25, alikua sehemu ya kikosi cha Mali kilichoshiriki fainali za Afrika zilizochezwa nchini Gabon mapema mwaka huu.

Anaihama Stade  Reims, baada ya kuitumikia katika michezo 32 msimu uliopita, jambo ambalo lilimuwezesha kuaminiwa na benchi la ufundi la klabu hiyo pamoja na mashabiki.

Kujiunga kwake na Rennes, kunampa nafasi ya kujumuika na waafrika wenzake Rais Mbolhi, Ramy Bensebaini na Mehdi Zeffane (Algeria), Edson Mexer (Msumbiji), Kermit Erasmus (Afrika Kusini), Firmin Mbule (DRC) na Giovanni Sio (Ivory Coast).

Traore tangu alipoanza maisha ya soka barani Ulaya akitokea nchini kwao Mali alipokua anaitumikia klabu ya JMG Bamako, ameshacheza michezo 120, ambapo alianzia Ubelgiji kwenye klabu ya Lierse mwezi July mwaka 2013, kisha alijiunga na Reims ya Ufaransa.

Video: Chadema wafunguka sakata la Makinikia, wasema JPM achukue hatua bila kubagua
Mrema ampa tano JPM, ashangazwa na baadhi ya wabunge