Jumuiya ya Kuhifadhi Qur-an Tanzania imetenga dola za kimarekani elfu 25 kwaajili ya washindi watakaoibuka kwenye mashindano ya kimataifa ya kusoma Qur-an ambayo yanayotarajiwa kufanyika siku ya Jumapili katika ukumbi wa Diamond Jubilee.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Sheikh Ally Kaporo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mashindano hayo ya sita kimataifa tangu yaanze kuratibiwa ambapo yanatarajiwa kushirikisha nchi 19 ambazo ni Kenya, Uganda, Mali, Nigeria, Algeria, South Africa, Bangladesh, Sudan, Kuwait, Libya, Djibouti, UAE, Russia Federation, USA, Yemen, UK, Dubai, Tanzania.

Amesema kuwa mgeni rasmi katika mashindano hayo anatarajiwa kuwa Makamu wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Iddy akiambatana na mlezi wa Jumuiya hiyo Alhaj Ally Hassan Mwinyi Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Hata hivyo, Sheikh Kaporo ametoa wito kwa watanzania kuhudhuria mashindano hayo na kujitokeza kwa wingi wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhani ambapo katika kumi la mwisho iliteremka Qur-an tukufu hivyo ni vyema wakahudhuria ili waweze kupata ujira kutoka kwa mola wao (Allah).

 

Video: Lowassa alitingisha tena Bunge Dodoma, Wabunge wataka maandamano
Arnaud Djoum: Tutapambana Kwa Niaba Ya Foe