Australia imesema kuwa itastisha operesheni yake ya mashambulizi nchini Syria kufuatia tishio lililotolewa na Urusi la kutaka kuzishambulia ndege za nchi hiyo endapo zitaendelea kutekeleza mashambulizi.
Onyo hilo la Urusi limekuja mara baada ya Marekani kuitungua ndege ya kijeshi ya Syria, huku Urusi ikisitisha mawasiliano na kuzuia visa ili kuonyesha kuwa haijafurahishwa na kitendo kilichofanywa na Marekani.
Australia imepeleka wanajeshi 780 kama sehemu ya muungano unaoongozwa na Marekani kupigana na kundi la Islamic State lililopo nchini humo kwaajili ya kurejesha amani ya nchini hiyo.
Hata hivyo, Australia inakikosi kidogo lakini ina ndege sita za F/A, Manowari ya kivita na ndege ya kutoa tahadhari na vifaa vingine vyenye uwezo wa hali ya juu katika kushambulia maeneo yasiyofikia kirahisi.