Mtoto aliyekuwa akinywa mafuta na sukari, Shukuru Kisonga (16) ameruhusiwa kutoka katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) baada ya kupatiwa matibabu na afya yake kuimarika.
Aidha, Shukuru alifikishwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Mei 16, mwaka huu akitokea Tunduru ambako aliripotiwa kuishi kwa kunywa mafuta, sukari na maziwa.
Baada ya kufikishwa MNH alifanyiwa uchunguzi na timu ya madaktari Bingwa na kubaini kwamba ana ugonjwa wa Selimundu pamoja na upungufu wa madini ya chuma na kwamba upungufu wa madini hayo ulisababisha anywe mafuta, sukari na maziwa.
“Kwakweli namshukuru Mungu, pia nawashukuru sana madaktari na wauguzi wa Muhimbili kwani hali ya mwanangu ilikuwa mbaya, alikuwa hawezi kula chochote zaidi ya kunywa mafuta, maziwa na sukari, lakini baada ya kupatiwa matibabu, afya yake imeimarika na sasa anaweza kula vyakula vyote,’’ amesema Mama Shukuru.
Hata hivyo, Awali mtoto Shukuru alipelekwa katika Hospitali ya Misheni Tunduru kwa ajili ya kupatiwa matibabu, lakini ugonjwa haukooneka na baadaye alipelekwa hospitali Nyangao mkoani Lindi