Baada ya kukaa nje kwa muda wa mwaka mmoja bila kushiriki mashindano yeyote katika mchezo wa tenesi, mchezaji nguli wa tenesi, Victoria Azarenka amejikuta akishindwa kutamba katika mchezo wake wa kwanza mbele ya Mjapan, Risa Ozaki.
Azarenka alianza vizuri kwa raundi ya kwanza dhidi ya Ozaki ambapo aliongoza kwa seti 6-3 kabla ya kupoteza dhidi ya Ozaki 6-4, 5-4 katika mchezo wa raundi ya kwanza na kumfanya Ozaki kuongoza.
Aidha, mchezaji tenesi huyo alipumzika kucheza mchezo huo mara baada ya kujifungua mtoto Desemba mwaka jana, hivyo kumlazimu kupumzika kwa muda mrefu kwaajili ya malezi.
Hata hivyo, baada ya michuano ya Malloca mchezaji huyo anatarajiwa kushiriki katika michuano ya wazi ya Wimbledon, inayotarajiwa kufanyika mapema mwezi ujao