Katika hali isiyokuwa ya kawaida inayoendela kujitokeza Mashariki ya Kati, Israel imeishambulia nchi ya Syria kwa madai kuwa nchi hiyo ilidondosha bomu katika kambi moja ya kijeshi ya Israel kwa bahati mbaya.

Israel imekuwa ikiishambulia Syria mara kwa mara wakati wa mzozo lakini imegoma kujiingiza katika machafuko yanayoendelea nchini humo.

Hata hivyo, Israel iliteka eneo la Golan lililopo kusini mwa Syria katika vita ya mwaka 1967 ambapo ilifanikiwa kulinyakua na kuwa eneo lake.

 

Polisi yatawanya maandamano ya 'mashoga' nchini Uturuki
Jeshi la Polisi latoa tahadhari kwa watumiaji wa barabara