Mshambuliaji Wayne Rooney huenda akaanzisha makato wa kurejea kwenye klabu yake ya zamani ya Everton, kwa lengo la kutimiza malengo ya kucheza mara kwa mara.

Gazeti la The Sun limeripoti kuwa, mshambuliaji huyo hana furaha ya kuendelea kuwa sehemu ya wachzaji wa Man Utd chini ya utawala wa meneja wa sasa Jose Mourinho, ambaye ameonyesha kutomtumia mara kwa mara.

Gazeti hilo limeibua taarifa nyingine kwa kudai kuwa, huenda mshambuliaji huyo akaondolewa kwenye kikosi cha Man Utd kitakachoelekea Marekani kwa ajili ya kambi ya kujiandaa na msimu mpya wa ligi.

Rooney aliihama Everton mwaka 2004, na kutimkia Old Trafford majuma kadhaa baada ya kikosi cha England, kuondolewa kwenye fainali za Ulaya za mwaka huo, ambapo mshambuliaji huyo alifunga mabao manne.

Hata hivyo mpango wa Rooney wa kutaka kuachana na Man utd na kurejea Goodison Park, umeanza kuwapa wakati mgumu viongozi wa Man Utd kwa kutafakari ada yake ya uhamisho wa kuondoka klabuni hapo, kufuatia mkataba wa miaka miwiwli uliosalia.

Rooney mwenye umri wa miaka 31, mpaka sasa ameshaitumikia Man Utd katika michezo 559 na kufunga mabao 253 huku akilipwa mshahara wa Pauni 250,000 kwa juma.

JPM: Sisafiri sasa hivi, lazima niwanyooshe kwanza, hizi safari zipo tu
?LIVE: Waziri Mkuu akitoa hotuba ya kuahirisha Bunge