Mtumbuizaji wa nyimbo za asili Tanzania, Saida Karoli amefunguka na kusema hakupotea kwenye ramani ya muziki isipokuwa alirudi alipotoka kutumbuiza jamii za chini kabisa, na alipofikia sasa anathubutu kujiita kuwa ni mmoja kati ya wanawake wapambanaji.

”Nilikuwa natumbuiza vijijini kabisa hasa katika vijiji ambavyo vina wasukuma wengi, ndio maana wengine walisema nauza pombe za kienyeji”. Amesema Saida Karoli

Saida amesema ilimbidi afanye hivyo kuwatumbuiza watu vijijini ili aendeshe maisha kwani bila hivyo watoto wake wangekufa njaa.

Ameeleza kuwa amekutana na changamoto nyingi sana pindi anahangaika huku na huko kutafuta ridhiki, ilifika wakati watu wengine waligoma kuamini kuwa ndiye saida.

Saida alijutia sana umaarufu wake huku hana kitu mfukoni, alitamani kuwa Saida Karoli ambaye hakuwahi kuimba Salome wala kujulikana katika jamii za kitanzania.

”Jina liliniletea dhihaka, dharau za wazi na kutukanwa ”. amesema Saida Karoli.

Kwa kuwa anafamilia ya watoto watano waliohitaji malazi, chakula na mavazi, alifuta machozi, na kuzishinda dhihaka na kuingia mtaani kuwatafutia riziki watoto wake kwa kutumbuiza vijijini humo.

 

Video: Coyo afunika na video mpya 'Itakucost', iangalie hapa
Video: Cheyo awararua Lowassa na Sumaye, DCI awaanika vigogo wapya kwenda Keko