Serikali ya Kenya imetangaza amri ya kutotembea usiku kwa muda wa miezi mitatu katika maeneo ya Lamu, Tana River na Garisa ili kuweza kuepusha mashambulizi ya mara kwa mara ambayo yamekuwa yakifanywa na wanamgambo wa Al -Shaabab.

Amri hiyo imetolewa na Kaimu Waziri wa Mambo ya Ndani wa Nchi hiyo, Fred Matiangi mara baada ya kukutana na Rais, Uhuru Kenyatta na baraza la usalama la taifa kujadili hali ya usalama.

Aidha, amri hiyo iliyotolewa imeanza rasmi hivyo mwisho wa kutembea usiku itakuwa ni saa 12:30 jioni mpaka saa 12:30 asubuhi ambapo watu wataruhusiwa kuendelea na shughuli zao.

Hata hivyo, amri hiyo imekuja mara baada ya siku ya Ijumaa kuuwawa kwa watu tisa kwa kuchinjwa katika maeneo hayo hali ambayo inahatarisha amani katika maeneo yaliyowekewa amri hiyo ya kutotembea usiku.

Mtandao haki za binadamu kupinga mahakamani Polisi kuzuia Maandamano
?LIVE: Rais Dkt. Magufuli akipokea nyumba 50 kutoka taasisi ya Mkapa