Wanasayansi na watafiti nchini New Zealand kutoka chuo kikuu cha Auckland wamefanya utafiti na kuvumbua chanjo yenye uwezo wa kudhibiti ugonjwa wa Kisonono.

Utafiti huu umefuatiwa na taarifa zilizosambaa siku chache zilizopita kuwepo uwezekano mkubwa wa ugonjwa wa kisonono kuwa moja kati ya magonjwa sugu yasiyo na tiba nchini humo, kwani tiba ambayo ilikua inapatikana ni ya kudumu kwa takribani miaka miwili tu.

”Kisonono kimekuwa tabu kutibika kwa sababu imezoea dawa za Antibiotic” amezungumza mmoja wa watafiti hao.

Watafiti wamebaini hayo baada ya kutoa chanjo hiyo kwa waathirika na matokeo kuonesha kuwa idadi kubwa ya wagonjwa waliotumia chanjo hiyo kupata nafuu na maambukizi kushuka kwa takribani theluthi moja.

Tafiti juu ya chanjo hizo zilipatikana baada ya vijana zaidi ya milioni moja kupewa chanjo ya ugonja wa kisonono  pindi walipoumwa wakiwa nchini humo.

Aidha madakatari nchini kote  wanashauri vijana na watu wote wanaoshiriki katika ngono zembe kuacha kabisa na kujikinga na magonjwa ya zinaa kama kisonono, kaswende na Ukimwi kwani ni hatari katika maisha yao.

”Kinga ni bora kuliko tiba” daktari mmoja amemalizia kwa kusema hivyo.

 

 

Prof. Maghembe aapa kula sahani moja na majangili
Peter wa P Square aitabiria haya ngoma mpya ya Vanessa