Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe amefunguka na kuwaomba wanachama wake kuwa na roho ngumu ya kupigania chama na kuachana na tamaa za pesa kwani endapo angekuwa na roho nyepesi basi angeshahama upinzani.
‘’Upinzani ni wito, wenye roho nyepesi hawawezi, kama kama ningekuwa napenda fedha nina roho nyepesi, ningeshachukua hizo pesa na ningeshakimbia kabisa upinzani, amesema mbowe.
Hayo ameyazungumza wakati madiwani saba wa Chadema tayari wamekwisharudisha kadi zao na kujiuzului chama jicho kwa kumuunga mkono Rais Magufuli.
-
Mbunge Chadema awaomba wananchi waliombee taifa
-
Majaliwa akabidhi magari mawili ya kubebea wagonjwa Ruangwa
Hata hivyo amewaomba viongozi wenye vyeo mbalimbali ndani ya chama hicho kuwa na roho ngumu na kuweka pembeni maslahi ya pesa kutokana na ugumu wa kazi, hivyo inahitaji uvumilivu mkubwa na kukubaliana na manyanyaso, maumivu, kudhalilika na kufungwa wakati wowote na kukosa ushirikiano hivyo ni kazi inayohitaji msimamo wa hali ya juu.
Aidha mpaka sasa madiwani wake wa Arusha wamekihama chama hicho, na jana ilikua zamu ya Diwani wa Ambuleni, Arumeru, Japhet Jackson.