Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita amefanya ziara ya kutembelea miradi ya Maendeleo ya jiji ambapo amesema kuwa ameridhishwa na vikundi vinavyo tengeneza mkaa kwa kutumia  malighafi ambayo itasaidia kupunguza uchafu uliopo kwenye maeneo mbalimbali na kuliweka jiji katika hali ya usafi.

Katika ziara hiyo ambayo imehusisha Kamati ya Fedha ya  Halmashauri ya Jiji, imetembelea vikundi vya Maendeleo ya ujasiriamali cha Upendo Smart kilichopo  mtaa wa Kilimahewa Kata ya Tandika kinachojihusisha na uzalishaji wa mkaa mbadala ( mkaa poa).

Aidha, amesema kuwa wananchi wanatumia gharama kubwa kununua mkaa unaochomwa kwa kutumia miti, lakini unapotumia huo ambao unatengenezwa na vikundi hivyo  kwa kutumia malighafi unaweza kusaidia kuinua uchumi.

“Mmefanya kazi nzuri sana wakina mama, nimeona juhudi zenu, lakini nimesikia changamoto kubwa hapa ya kuwafikia hao wateja ili waweze kununua nishati hii, niwahakikishie madiwani wenu wapo hapa, Meya wenu nipo hapa tutaendelea kuwaunga mkono,” amesema Mwita

Hata hivyo, ziara hiyo ilianzia kwenye  mradi wa ujenzi wa viwanda vidogo vidogo katika eneo la karakana Mwananyamala ambapo lengo la mradi huo ni kuwahudumia wananchi na wajasiriamali wadogo wadogo ili kuinua hali ya uchumi.

 

Real Madrid kujaribu mara ya mwisho, yatenga dau nono
Gerard Pique atamba kutwaa ubingwa wa Hispania, Ulaya