Mtu mmoja ameuawa nchini Venezuela wakati akisubiri kupiga kura ya maoni liliyoandaliwa na upinzani dhidi ya mipango ya Serikali kuandika upya katiba ya nchi hiyo ili iweze kuendana na wakati.
Watu wasiojulikana waliokuwa na silaha wamewashambulia wapiga kura nje ya kituo cha kupigia kura nje ya mji mkuu wa nchi hiyo Caracas, huku wengine watatu wakijeruhiwa vibaya na kukimbizwa hospitali.
Aidha, Mpaka sasa idadi kubwa ya watu wamefariki dunia katika ghasia ambazo zimeelezwa kuwa ni mbaya zaidi kutokea nchini humo na zimeathiri pakubwa uchumi wa nchi hiyo na jitihada za Rais  Nicolas Maduro kung’ang’ania madarakani.
-
Ndege ya jeshi la Marekani yaanguka na kuua 16
-
Trump ajitathmini, aanza kulegeza misimamo yake
-
Rais wa Brazil kikaangoni, Bunge lamkingia kifua
Hata hivyo, Mwezi May mwaka huu, Rais Maduro alitoa agizo la kufanyiwa kwa marekebisho ya katiba, kitendo ambacho kilipingwa vikali na wapinzani kwa madai kuwa ni kinyume na demokrasia.