Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi ( CUF) anayaetambuliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini, Prof. Ibrahim Lipumba amevitaka vyombo vya dola kumchukulia hatua kali mwanachama wa chama hicho, Bashange kwa kuingilia majukum ya Naibu Katibu Mkuu Bara, Magdalena Sakaaya.

Ameyasema hayo mapema hii leo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema kuwa mwanachama huyo anastahili kuchukuliwa hatua kali kwakuwa anavunja Katiba ya Chama hicho.

“Bashange anavunja Katiba ya Chama chetu kwa kujifanya yeye ni Naibu Katibu Mkuu Bara, wakati nafasi hiyo ni ya Magdalena Sakaaya, hivyo naviomba vyombo vya dola vimchukulie hatua kali,”amesema Prof. Lipumba.

Aidha, katika hatua nyingine Prof. Lipumba amemsimika Magdalena Sakaya kukaimu nafasi ya Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad mpaka hapo atakapoanza kutimiza majukumu yake.

Makamba afanya ziara ya ukaguzi wa ujenzi wa kingo za fukwe jijini Dar
Serikali kuimarisha uhusiano na vyombo vya habari nchini