Jeshi laPolisi Kanda Maalum ya Dar es salaam limekamata vifaa mbalimbali vya magari vilivyoibiwa mara baada ya kufanya operesheni kali kwa muda wa siku saba kama lilivyokuwa limeagizwa na mkuu wa mkoa huo.

Katika operesheni hiyo jumla ya watuhumiwa 73 walikamatwa na vifaa vya Magari vilivyoibiwa ikiwmo Power Window 40, Radio 12, Taa za Magari 105, Side Mirrors 92, Vitasa vya Magari 109, Bampa 4, Air Cleaner 1, Booster 3, Show Grill 6, Mashine moja ya kupandisha vioo na Tyre zilizotumika 2.

Hayo yasemwa mapema hii leo na Kaimu Kamishna wa Kanda Maalum ya Dar es salaam, Kamanda Lucas Mkondya alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amewataka wananchi wa mkoa huo kufika Kituo Kikuu kwaajili ya kurudishiwa vifaa vyao bila malipo.

Aidha Makonda ameliagiza tena Jeshi la Polisi kusambaratisha wafanyabiashara wa magari (Madalali) wanaofanya biashara ya kuuza magari katika maeneo yasiyo rasmi na kusababisha serikali kukosa mapato.

“Watuhumiwa wote bado wanaendelea na mahojiano na uchunguzi bado unaendelea ili kubaini mtandao wote unaojihusisha na wizi huo wa vifaa hivyo vya magari ikiwa ni pamoja na kuwafikisha mahakamani kwa hatua zaidi,” amesema Mkondya.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda ameliagiza Jeshi hilo kutokomeza maeneo ambayo yamekuwa yakitumika kama bandari Bubu na kusambaratisha wezi wa Magari ambao pia wamekuwa wakiiba Magari na kuuza kifaa kimoja kimoja.

 

Video: Boda Boda Wilaya ya Ilala waandamana kumpongeza JPM
Waziri Mkuu Azindua Meli mbili zilizonunuliwa na Serikali Mkoani Mbeya