Mshambuliaji Carlos Tevez amelazimika kurejea nchini kwao Argentina kwa lengo la kujiuguza majeraha ya kiazi cha mguu, huku akitarajiwa kurejea China kujiunga na wachezaji wenzake wa Shanghai Shenhua, kabla ya mwishoni mwa mwezi huu.
Tevez aliutaka uongozi wa klabu yake kumruhusu kurejea jijini Buenos Aires, ambapo anaamini atapata muda wa kutulia na familia pamoja na kujiuguza jeraha ambalo litamchukua muda wa majuma mawili kupona.
Hata hivyo, inadaiwa kuwa mshambuliaji huyo wa zamani wa klabu za West Ham Utd, Man Utd, Man City na Juventus, atakuwa chini ya uangalizi wa daktari wa klabu ya Boca Juniors, ambayo ilikubali kumuuza mwanzoni mwa mwaka huu kwa ada ya Pauni milioni 12.93.
-
Mkongwe Wa Ligi Ya England Kuhamia The Hawthorns
-
Mfumo washindwa kuhimili kamali ya pambano la Mayweather Vs McGregor
Tevez alisaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia klabu ya Shanghai Shenhua na tayari ameshacheza michezo 11 na kufunga mabao mawili.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 33, hakucheza michezo miwili iliyopita, na anatarajiwa kukosa mchezo wa kesho wa kombe la chama cha soka nchini China (Chinese FA Cup) dhidi ya klabu ya ligi daraja la pili, Shanghai Shenhua.
Pia, ataukosa mchezo wa ligi utakaochezwa jumamosi dhidi ya mabingwa watetezi Guangzhou Evergrande.