Jengo la Mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania Bara, Klabu ya Yanga linatarajia kupigwa mnada hapo kesho ili kufidia deni ya kodi ya ardhi inayodaiwa Klabu hiyo kiasi cha shilingi milioni 300.

Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi imetangaza kupigwa bei kwa jengo hilo kufuatia kesi iliyofunguliwa na Kamishna wa Ardhi katika Baraza la Ardhi Wilaya ya Temeke na Ilala dhidi ya Klabu hiyo iliyoanzishwa mwaka 1935.

Aidha, katika tangazo lililotolewa na Kampuni ya udalali ya Msolopa Investment imesema kuwa mnada wa kulipiga bei jengo hilo umepangwa kufanyika kesho jumamosi kuanzia saa nne asubuhi Klabuni hapo.

“Kuna makosa kidogo yametokea kwenye uhariri kwenye tangazo, tunarejea mahakamani kuripoti kilichotokea, kisha tutawajulisha kwani tarehe ilikuwa ni 17, Agosti, kwenye gazeti imeandikwa tarehe 19, Agosti mwaka huu, hivyo jumamosi tutatekeleza mnada huo,”amesema Msolopa.

Hata hivyo, Katibu Mkuu wa Klabu ya Yanga, Boniface Mkwasa amekiri kudaiwa kwa Klabu hiyo zaidi ya milioni 300 huku akisema zinatokana na malimbikizo ya deni la kodi ya majengo na ardhi.

Video: Makonda aibua upya vita dawa za kulevya, Kitimtim mnada jengo la Yanga
Grace Mugabe atoweka Afrika Kusini, Polisi wahaha kumsaka