Rais wa Rwanda, Paul Kagame amesema kuwa Afrika inatakiwa kujiwekea misingi yake yenyewe ya kiutawala lakini si kuiga mifumo ya nchi za magharibi ambayo imekua ikiharibu tamaduni zote.

Ameyasema hayo katika hotuba yake mara baada ya kuapishwa kuiongoza tena nchi hiyo kwa muda wa miaka saba, ambapo amewaasa viongozi wa Kiafrika kupigania kujiwezesha kwa mataifa yao kama anavyofaya yeye.

“Tulilazimika kupambana ili kulinda haki zetu na kufanya kile ambacho ni kizuri kwetu na tutaendelea kufanya hivyo. lakini Rwanda haiwezi kuwa mfano pekee lazima kila mwananchi wa Afrika, kila taifa lipiganie kuishi bila kuetegemea wengine au bila kujali wengine wanavyotaka. Wanataka mifumo inayofanya kazi vizuri kwetu tuibadilishe na mifumo yao ambayo wananchi wao wameanza kupoteza imani nayo.”amesema Kagame

Aidha, Kagame amesema kuwa miaka 23 baada ya Rwanda kukumbwa na mauaji ya kimbari wananchi wake waliamua kujenga taifa linalojiwezesha lenyewe bila kutegemea nchi za nje.

Hata hivyo, mara tu baada ya uchaguzi huo kumalizika Marekani ambaye ni mshirika wake wa karibu wa Rwanda licha ya kuwapongeza wananchi wa Rwanda kwa uchaguzi nchi hiyo ilisema kulikuwa na dosari zilizojitokeza kabla na wakati wa uchaguzi.

Makonda kuendesha kampeni kujenga nyumba 402 za walimu Dar
Video: Lissu aizulia jambo Bombardier, Ugonjwa wa Manji selo waahirisha kesi yake