Wananchi wa Mji wa Kibaha Mkoani pwani wameilalamikia kampuni ya M/S Group Six LTD inayojenga Stendi mpya ya mabasi kuwauzia kifusi cha mchanga ambacho halmashauri ya mji huo ilitoa bure kwa wananchi ili kupisha ujenzi wa kituo hicho.

Kwamujibu wa mwananchi aliyejitambulisha kwa jina la Rashid Kajumbo kutoka kampuni mzawa wa MEG Business Solution amesema kuwa kuwa Wachina hao wamekuwa wakiwatoza kiasi cha shilingi Elfu 5,000 hadi elfu 20,000 ili kupata kifusi hicho jambo ambalo ni kinyume cha agizo la mkurugenzi wa  Halmashauri ya Mji wa Kibaha.

Aidha, Rashid ambaye tayari alikuwa na kibali cha mkurugenzi mkononi cha kupewa kifusi hicho bure amesema magari yake manne yaliyopo katika eneo la mradi wa Stendi hiyo inayojengwa karibu na Karakana ya Serikali hato yaondoa mpaka Waziri Mkuu, Kasimu Majaliwa atakapofika katika eneo hilo na kuelezwa jambo hilo.

Hata hivyo, Dar24.com ilimtafuta Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kibaha, Jenifa Omolo kwa njia ya simu ambaye amesisitiza kuwa hafahamu chochote kuhusu hilo ingawa anatambua kifusi hicho kinatakiwa kutolewa bure na hivyo amesema kuwa atafuatilia suala hilo ili kujua kama Kampuni hiyo inawauzia wananchi kifusi hicho.

 

 

 

 

 

Magazeti ya Tanzania leo Agosti 27, 2017
Video: Mahakama imetenda haki- Sakaya