Korea Kaskazini imeigeuzia ubao nchi ya Japan mara baada ya kufanya Jaribio la silaha za nyuklia za masafa marefu yaliyokatiza katika anga la Japan hali ambayo ilizua taharuki kwa wananchi na viongozi wa nchi hiyo.
Makombora hayo yalisafiri karibia kilomita elfu moja mashariki mwa kisiwa cha Hokkaido kilichopo nchini Japan kabla ya kudondoka mashariki mwa bahari ya nchi hiyo kitu ambacho kimeishtua Japan.
Aidha, tukio hilo limechochea tahadhari ya hatari ambayo watu walielekezwa kujificha katika maeneo yaliyo chini ya ardhi ama kwenye majengo yaliyojengwa imara ili kuweza kujinusuru na hatari ambayo ingeweza kujitokeza.
Waziri mkuu wa Japan, Shinzo Abe amesema kuwa urushwaji huo wa makombora ambao haujawahi kutokea, umeleta hisia tofauti na kitisho kikubwa kwa taifa lake ambalo halijawahi kuwa na mgogoro na nchi hiyo.
Hata hivyo, Wanajeshi wa Marekani na Japan wanaendelea kufanya mazoezi ya pamoja katika eneo hilo la Hokkaido, huku rais wa Korea Kusini, Moon Jae-in akitaka kujibu shambulio hilo kwa nguvu za kijeshi.