Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi (SACP), Lazaro Mambosasa amewataka wananchi kutoa ushirikiano kwa jeshi la Polisi ili liweze kukabiliana vyema na kukomesha uhalifu jijini humo.
Ameyasema hayo mapema hii leo jijini Dar es salaam alipokuwa akijitambulisha mbele ya waandishi wa habari baada ya kuitikia wito wa uteuzi alioupata hivi karibuni, amesema kuwa ushirikiano kati ya jeshi hilo na wananchi ni njia pekee ambayo itasaidia kukomesha uhalifu jijini Dar es salaam.
“Mimi niwaalike wakazi wa Dar es Salaam wote kuwa kila mtu amwangalie mwenzake katika masuala ya uhalifu, ila suala la utekaji nyara watu mkiwa mnafikiria ni tatizo la jeshi la polisi pekee yake mtakuwa mnakosea. Kila mmoja wetu anaweza akawa mtekwaji mtarajiwa kwa hiyo tusikubaliane na uhalifu tuwafichue hao watu,”amesema Mambosasa
Aidha, amesema kuwa katika utekelezaji wa majukumu yake huwa anaamini kazi nzuri ile ambayo imewashirikisha wananchi wa eneo husika hivyo amewaa wananchi wote kutoa ushirikiano mkubwa kwa jeshi hilo.
-
Mjamzito aishitaki hospitali ya Kairuki kumsababishia utasa
-
Rais Magufuli alivyotembelea makao makuu ya Kakukuru
-
Kamati ya Bunge yafanya ziara Muhimbili, Dart na IFM
Hata hivyo, Mambosasa ameongeza kuwa Jiji la Dar es Salaam ni kubwa kuliko mingine hivyo atahakikisha anakomesha uhalifu na kuwafanya wananchi kuishi kwa amani bila hofu yeyote.