Tasnia ya Habari imekumbwa na msiba baada ya kuondokewa na gwiji wa habari, Muhingo Rweyemamu aliyefariki Dunia saa tatu asubuhi jana katika Hospitali ya Agakhan D’Salaam alipokuwa akifanyiwa matibabu.

Marehemu alikuwa akisumbuliwa na  ugonjwa wa Myelofibrosis ambao hudhoofisha uwezo wa kinga za mwili kutengeneza damu, hivyo hupelekea mwili kuwa na kiwango cha chini cha kutengeneza damu hali ambayo husababisha mwili kuwa na upungufu wa damu mara kwa mara.

Akizungumza msemaji wa familia ambaye ni kaka yake Muhingo amesema ” Kwa kipindi kirefu takribani miaka 11 iliyopita, Muhingo alikuwa akiumwa na kuwekewa damu mara kwa mara na mwaka jana ndipo alipozidiwa na tulimpeleka katika vituo vya afya zikiwemo hospitali kubwa kwa matibabu, kama vile Muhimbili, India, na Agakhan na kwa mujibu wa daktari waliokuwa wanampatia matibabu , wamesema maradhi hayo hayana tiba”.

Marehemu alikuwa akitumikia tasnia ya uandishi wa habari na ametumikia magazeti mbalimbali nchini na baadaye kuwa Mhariri Mtendaji wa kampuni ya New Habri (2006) ltd.

Hata hivyo wafanyakazi wenzake wanasikitika kutangaza kifo hiko kwani wanaamini tasnia imepoteza silaha kubwa, Muhingo alikuwa na uwezo mkubwa katika lugha ya kiswahili na kingereza.

”Ni siku ya huzuni na maombolezi tumepoteza mmoja wa wanahabari mwenye maarifa mengi na kiwango chake si cha kutilia shaka, ameacha urithi mkubwa” amesema Absalom Kibanda ambaye ni mtendaji katika kampuni ya New Habri (2006) ltd.

Aidha familia bado inaendelea na taratibu za mazishi kwa kufanya vikao vya wanandugu ili kupanga mahali na siku ya kupumzisha mwili wake.

Uongozi na wafanyakazi wa Dar24 unapenda kutoa pole za dhati kwa wanafamilia, ndugu, jamaa, na wafanyakazi wote wa marehemu, Mungu aipumzishe kwa amani roho ya Muhingo Rweyemamu.

 

 

Msuva amtaja Samatta kuwa chachu ya mafanikio yake kisoka
Kenyatta: Majaji waliobatilisha matokeo ni wakora