Wanafunzi 37 wa Shule ya Sekondari Milambo ambao walikuwa wamefukuzwa kwa kosa la kutoroka na kutokuwepo kwa maeneo ya Shule usiku wamesamehewa na Bodi ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora na kutakiwa kutafuta Shule nyingine za kuhamia.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Rufaa ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri alipokuwa akizungumza na wazazi, amesema kuwa kutokana na maelezo ya wanafunzi na wazazi waliona kuwa Bodi ya Shule ya Sekondari Milambo ilikuwa sahihi kuwafukuza.
Amesema kuwa Bodi ya Rufaa ilifikia uamuzi huo wa kuwasaheme baada wanafunzi na wazazi wao kukiri makosa na kuomba msamaha pia kufanya majadiliano na kwa mawasiliano ya karibu na ile ya Shule ndipo walipoamua kuwasaheme kwa masharti ya kuwa wahamie sehemu nyingine ili wamalizie masomo yao.
Aidha, Mwenyekiti huyo wa Bodi ya Rufaa amesema kuwa baada ya msamaha huo wanafunzi hao hawataruhusiwa kurudi Milambo badala yake wazazi na wanafunzi hao watalazimika kutafuta Shule za kuhamia ambapo uongozi wa Mkoa na ule wa Shule utawasaidia kuwaandika barua na kuwajazia fomu zitakazohitajika.
-
Video: Tumemchoka Mange – DCI, Magufuli awaonya viongozi wastaafu
-
Video: IGP Sirro apokea hundi ya shilingi milioni 120 kutoka SportPesa
-
Serikali kuanzisha Fao la Upotevu wa Ajira
Hata hivyo, kwa upande wake Katibu Tawala Msaidizi Mkoa wa Tabora anayeshughulikia Elimu Suzana Nussu aliwaomba vijana hao ambapo wamepata msahama huo wa Bodi kufuata mambo ambayo yamewapeleka Shuleni ili waweze kumaliza bila matatizo.