Kamati ya nidhamu iliyokutana Jumapili Januari 14, 2018 imepitia kesi ya mshambuliaji wa Yanga Obrey Chirwa iliyowasilishwa na Bodi ya Ligi iliyohusu mchezo namba 83 kati ya Yanga na Tanzania Prisons iliyochezwa Novemba 25, 2017 Uwanja wa Azam Complex.
Chirwa alishtakiwa kwa kosa la kumpiga mchezaji wa Tanzania Prisons kwenye mchezo huo uliomalizika kwa sare ya kufungana bao 1-1.
Chirwa ambaye alifika kusikiliza kesi hiyo akiwa na muwakilishi wake alikiri kutenda kosa hilo.
Kamati baada ya kumsikiliza Chirwa na kupitia Video za mchezo huo pamoja na taarifa ya kamishna na Muamuzi imetoa adhabu kwa mchezaji huyo kupitia Kanuni za Ligi Kuu kanuni ya 37(7b) na kanuni za nidhamu za TFF kifungu cha 48(1d) na 48(2).