Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe ametoa wito kwa watanzania kujitokeza kumchangia msanii wa Filamu, Wastara Issa ili aweze kwenda kupatiwa matibabu India ya mguu wake unaomsumbua.

Ametoa wito huo hii leo Jijini Dar es salaam alipokwenda kumtembelea msanii huyo wa filamu nyumbani kwake Tabata Sanene kutokana na msanii huyo kuwa anasumbuliwa na mguu wake uliokatwa mpaka kufikia kuhitajika kufanyiwa upasuaji mwingine.

“Ndugu zangu watanzania najua kutoa ni moyo na siyo utajiri ninawaomba mjitokeze kwa kumsaidia msanii huyo kwani mpaka sasa anahitaji kiasi cha milioni kumi na nane kwa ajili ya kufanikisha safari yake hiyo ya kwenda kupata matibabu na anatarajia kwenda kwenye matibabu hayo mwezi ujao,” Dkt.Mwakyembe.

Naye Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania, .Joyce Fissoo ametoa wito kwa wasanii wote wa filamu nchi kujitokeza na kumsadia mwanatasnia mwenzao wa filamu katika kufanikisha anapata matibabu ili aweze kurudi na kuendelea kufanya kazi zake kama kawaida

Hata hivyo, kwa upande wake Katibu Mtendaji BASATA, Godfrey Mngereza ametoa wito kwa wasanii wote nchini kujitokeza kumchangia msanii huyo kwani wasanii wote ni wamoja kwa maana wote wanafanya kazi ya sanaa hivyo ni vyema kuwa na mshikamano na kusaidiana.

 

Nuru The Light: Kuna watu..., aliponiacha nikaona Diamond
Majaliwa aagiza Wakurugenzi wachunguzwe