Sam wa Ukweli ameweka wazi kilichomfanya awe kimya kwenye mkondo mkuu wa muziki wa Bongo Fleva kwa miaka kadhaa baada ya kutikisa na ‘Sina Rana’ na ‘Hata Kwetu Wapo’.
Mwimbaji huyo aliyetembelea studio za Dar24 na kuweka mambo hadharani kupitia mahojiano maalum, amesema kuwa ukata ulioivamia kampuni iliyokuwa inasimamia kazi zake za muziki ulisababisha akwame kuendelea na sanaa kwa muda.
Alisema baada ya kuona wasimamizi wake wamekumbwa na ukata huku akiwa amefungwa pingu ya mkataba wa miaka mitatu, aliona asiingie kwenye mgogoro wa kimkataba kama ilivyokuwa kwa mtangulizi wake kwenye usimamizi huo, Diamond Platinumz.
Sam wa Ukweli ambaye amerejea kwenye game na wimbo wake mpya ‘Milele’, alifunguka sababu za kuamua kuchagua maisha ya kilimo cha mananasi na jinsi mambo yalivyokwenda baadaye. Kwa mamtiki hiyo, ni kama Sam aliufuata utajiri wa ardhi kwenye kilimo kama walivyofanya wasanii wengine kama Masanja Mkandamizaji na Dogo Ditto.
Pia, mwimbaji huyo amefunguka kuhusu kinachoelezwa kuwa ni mgogoro kati yake na Meneja Maneno aliyeamua kufanya kazi na Rich Mavoko.
Angalia mahojiano yote hapa upate kwa undani na usisahau ku-subscribe.