Nchini Kenya mamia ya wanafunzi katika shule ya Sekondari ya Jamhuri jijini Nairobi wameingia katika mvurugano mkubwa kufikia hatua ya kuchomana visu baada ya usiku wa jana kutokea vurugu ya kidini kwenye shule yao.
Ambapo vyombo vya habari nchini humo vimeripoti taarifa hiyo na kueleza kuwa ugomvi huo umetokea kati ya wanafunzi wa kiislamu na wakikristu ambao walikuwa wakibishana kuhusu dini zao..
Kwenye mzozo huo Wanafunzi wa dini ya Kiislamu walikuwa wanawalazimisha wenzao wakristo kubadilisha dini (Kuslimu) na ndipo vurugu zilipoanzia.
Taarifa za awali zinaeleza kuwa vurugu hizo zimetokea usiku wa kuamkia leo na mamia ya Wanafunzi wamejeruhiwa kwa kuchomwa visu huku vitanda na madawati yakivunjwa kwenye vurugu hizo.
Hata hivyo tayari Jeshi la Polisi jijini Nairobi limefika shuleni hapo asubuhi hii kufuatilia tukio hilo ili kutoa taarifa rasmi idadi ya wanafunzi waliojeruhiwa.