Serikali ya Kenya imepiga marufuku uuzaji wa Parachichi nchi za nje kufuatia upungufu mkubwa wa matunda hayo ambayo yanapendwa sana nchini humo.

Kwa mujibu wa mtandao wa Citizen Digital, mratibu wa mamlaka ya kilimo na chakula ya Kenya (AFA), Alfred Busolo amesema kuwa parachichi ni tunda muhimu ambalo Wakenya wengi wanatumia wanapokula chakula.

Aidha, AFA imesema kuwa upungufu uliopo unatokana na kuwa huu sio msimu wa Avocado zinazopendwa aina ya Faurte na Haas.

Ripoti iliyochapishwa katika jarida la Bussines Daily Nation la Kenya mapema wiki hii, imesema kuwa kilo 90 za tunda hilo ilikuwa zinagharimu shilingi 2,560 za Kenya kufikia Disemba 2017.

 

Rais Kagame kuteta na Trump kuhusu Afrika
Magazeti ya Tanzania leo Januari 25, 2018