Jumba la Makumbusho la Guggenheim lililoko jijini New York nchini Marekani limeiambia Ikulu ya nchi hiyo kuwa liko tayari kutoa ‘choo cha dhahabu’ kwa mkopo kwa ajili ya Rais Donald Trump ikiwa ni mbadala wa ombi la mchoro wa zamani lililowasilishwa kwao.

Awali, Ikulu ya Marekani iliomba jumba hilo liwape mchoro wa msanii wa Italia, Vincent Van Gogh wa karne ya 19 kwa ajili ya kuuweka kama pambo la Ikulu, lakini ombi hilo lilikataliwa kwa maelezo kuwa hauwezi kuondolewa kwenye jumba hilo.

Kwa mujibu gazeti la The Washington Post, mhifadhi wa jumba hilo Nancy Spector alituma barua pepe kwenda ikulu Septemba mwaka jana akiomba radhi kwa kutopatikana kwa mchoro huo huku akiwapa ahadi ya mkopo wa choo hicho endapo wataridhia.

“Ingawa choo hiki kilikuwa kinatumiwa na wageni wetu, lakini kinapatikana kama Rais na Mke wake wataridhia, tutawapa kwa mkopo wa muda mrefu,” inasomeka sehemu ya barua pepe hiyo kwa mujibu wa The Washington Post.

Choo hicho cha dhahabu kina thamani ya zaidi ya dola za kimarekani 1,000,000 ($1 million) na kimetengenezwa kwa karati 18 za dhahabu.

Mr. Blue akanusha 'kumdiss' Ali Kiba
Mfanyabiashara aliyekutwa na fedha za kigeni kinyume na sheria afikishwa kizimbani