Mwanariadha mwenye kasi duniani Usain Bolt, amejiunga na kufanya mazoezi na timu ya mpira wa miguu Mamelodi Sundowns ya nchini afrika kusini mapema wiki hii.
Raia huyo wa Jamaica anaye shikiria rekodi ya dunia kwa kushinda medali za dhahabu mara nane kwenye mashindano ya Olimpiki kwenye mbio za mita 100 na mita 200 ,Ametembelea nchi hiyo ikiwa ni sehemu ya mpango wa kukuza michezo.
Bolt ambaye amestaafu kukimbia baada ya mashindano ya mabingwa wa dunia yaliyofanyiika jijini London mwezi agosti mwaka jana ni shabiki mkubwa wa timu ya Manchester United na mara kadhaa amekuwa akizungumzia dhamira yake ya kucheza soka.
Baada kushiriki mazoezi na mabingwa hao wa Afrika 2016, Bolt amesema anayo furaha furaha kushiriki mazoezi na timu hiyo huku akiahidi kuendelea kujiweka fiti pindi atakapo rudi nchini kwako Jamaica.
-
Arsenal yakaribia kumnasa Aubameyang
-
Conte adai anafuraha kuendelea kuinoa Chelsea
-
Manara aihofia Maji Maji
Hata hivyo, mwanariadha huyo nguli duniani mwezi Machi amealikwa kushiriki mazoezi na timu ya Borussia Dortmund inayoshiriki ligi kuu ya Ujerumani Bundesliga