Zoezi linaloendelea nchini Kenya ni kwamba kiongozi wa Muungano wa Upinzani, Raila Odinga na makamu wake Kalonzo Musyoka wanatarajiwa kuapishwa leo katika viwanja vya uhuru.
Serikali imeamua kuzima baadhi ya vyombo vya habari vikiwemo televisheni na radio kukokurusha matanagazo ya kuapishwa kwa Raila Odinga.
Hata hivyo serikali imeruhusu kutumia uwanja huo, na kuwataka askari polisi waondoke mitaani na kuwaacha huru wafuasi wa NASA.
Wafuasi wa NASA wameonekana wakifurika kwenye viwanja hivyo kutoka sehemu mbali mbali za nchi ya Kenya, lakini mpaka sasa viongozi hao wawili hakuna aliyejitokeza uwanjani hapo.
-
Video: Mizinga ya nyuki yanaswa kwenye uwanja wa ‘kumuapisha’ Raila
-
Kenyatta: Ole wake atakayerusha mubashara kuapishwa kwa Odinga
Taarifa zaidi zinasema waandishi waliokwenda nyumbani kwa kiongozi wao Raila Odinga wamezuiwa kuzungumza naye, baada ya wanafamilia kusema ‘Baba’ hayupo.
Ifahamike kwamba iwapo Raila Odinga na Kalozno Musyoka watafanikiwa kuapishwa, watakuwa wamefanya kosa la uhaini na jaribio la kupindua Rais aliyepo, kwani yupo kwa mujibu wa Katiba ya nchi ya Kenya na ameapishwa kisheria