Diamond Platinum awafungukia mashabiki wake na kuwaeleza kuwa yeye na Wema ni washikaji wakubwa kwani ana amini kuwa wamekuwa watu wazima wanaosapotiana katika kazi mbalimbali za sanaa.
Amedai kuwa hawawezi kuwa na uhasama milele inafika kipindi watu wanakuwa na kuweka tofauti pembeni huku wakiendelea na maisha mengine.
Aidha Diamond amechukizwa na kitendo cha mashabiki wake kumtolea maneno mabaya kwa kitendo cha kumwalika Wema Sepetu katika shughuli yake ya utambulsiho wa Mbosso katika kundi la WCB.
-
Diamond ampokea Wema kikuza sauti na ‘I love you die’
-
Gumzo: Diamond amtuliza Wema kifuani hadharani
Hivyo Kupitia ukurasa wake wa instagram ameandika haya
Wengi Hupenda kuona watu wakiwa wana Vita ama uhasimu usio na kichwa wala miguu… Eti utamsikia mtu anasema “Dogo Mi shabiki yako Mkubwa na nakukubali sana ila kitendo cha kumualika Wema Umeniuzi” kwaio we unataka mie niendelee kuwa na vita ama niwe na vita na Wema ili iweje? yani mie nikiwa na vita na Wema we unafaidika nini? na itanisaidia ama kusaidia nini kwenye Sanaa yetu? Huwezi kuwa shabiki yangu halaf unafurahia mie kuendelea kuwa na vita na mtu, tena vita ambayo imeshaisha…nina familia yangu Naipenda Naiheshimu na siwezi kuiacha… ila hio sio sababu ya kuwa na vita na watu…na huu ni mfano wa kwanza mwingine unafata…. Huu sio Muda wa kujenga chuki zisizo za msingi ni wakati wa wasanii kushirikiana na kwa pamoja kufanya kazi na kukuza sanaa zetu kwajili ya future ya wadogo na vizazi vyetu vijavyo… Shukran sana Mdam kwakuja usiku wa jana…Mwenyez Mungu akubariki na akujalie kila la kheri uliombalo