Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amekataa wito wa chama chake unaomtaka kujiuzulu akidai kuwa amezingatia maelekezo yote ya kisheria na hawezi kuachia madaraka hayo.
Rais huyo amekuwa akishinikizwa kujiuzulu kufuatia mazungumzo na maafisa wa ngazi ya juu katika chama chake cha ANC siku ya Jumapili.
Ambapo mazungumzo hayo hayakuwekwa wazi hasa yalihusu nini .
Taarifa hiyo imetolewa na Kiongozi wa Upinzani , Julius Malema aliyekuwa mfuasi wa chama hicho cha ANC, ambapo ametumia ukurasa wake wa Twitter kutoa taarifa hiyo, Juu ya Zuma kukataa kujiuzulu.
“Alikataa kujiuzulu na amewaambia wafanye uamuzi wa kumtoa kama watapenda kufanya hivyo kwa sababu hakuwa na hakuna kitu chochote kibaya alicho kifanya kwenye nchi hiyo. Analalamika kuwa alikubali maelekezo yote ya kisheria ikiwa ni pamoja ya kulipa fedha, Je, wanataka nini zaidi kutoka kwake.” Malema wa EFF aliandika katika akaunti yake ya Twitter.
Zuma aliyefungwa gerezani baada ya kushiriki katika vita dhidi ya ubaguzi wa rangi anaonekana kuwa katika hatua za mwisho za Urais.