Rais Mstaafu wa awamu ya pili Mh. Al Hassan Mwinyi anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye mchezo wa kimataifa dhidi ya Gendarmerie Nationale FC kutoka Djibouti.
Akizungumza na vyombo vya habari Mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano Haji Manara alisema ‘Tunategemea kuwa Mzee wetu, Rais wa awamu ya pili Al Hassan Mwinyi kuwa mgeni rasmi wa mchezo wetu dhidi ya Gendarmerie Nationale FC kwenye michuano ya kombe la shirikisho la CAF, mchezo huu ambao utachezwa Jumapili saa 10:00 jioni katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam’
Akiendelea kuelezea maandalizi ya mchezo huo alitoa taarifa ya kuja kwa timu ya Gendarmerie Nationale FC ambapo watawasili Jumamosi saa 7:00 usiku ukiwa ni msafara wa wachezaji 18 pamoja na viongozi 8.
Viingilio vya mchezo huo vitakuwa ni 30,000 kwa VIP A, 20,000 VIP B, Orange 10,000 na 5,000 kwa mzunguko.