Rais wa Ufilipino, Rodrigo Durtete ameamuru kuharibiwa kwa magari ya kifahari yanayokadiriwa kuwa na thamani ya zaidi ya US 1.2 million baada ya kuingizwa kinyemera nchini humo.
Aidha, Magari yameharibiwa kwa kutumia mashine aina Katapila, na baada tu ya kumalizika kwa zoezi hilo, rais huyo alikagua na kujiridhisha kama yote yameharibiwa.
“Huu ndio ujumbe kwa waingizaji bidhaa za thamani nchini bila kulipia ushuru na mapato,”amesema Durtete
Aidha, aina za magari yaliyoharibiwa ni pamoja na BMW, Jaguar, Mercedes Benzi na Corvert yote yameharibiwa katika bandari tatu tofauti nchini humo.