Mkuu wa Mkoa Manyara, Alexander Mnyeti amelivunja baraza la kata ya Murray, Wilayani Mbulu, baada ya wananchi kulalamika kunyanyaswa, kombwa rushwa na kunyimwa haki zao.
Kufuatia malalamiko hayo amemwambia Mkurugenzi Halmashauri ya Mji wa Mbulu, Anna Mbogo kuanza mchakato wa kupatikana kwa viongozi wapya wa baraza la kata hiyo..
”Kuanzia sasa hivi, hilo baraza nimelivunja sitaki kuliskia tena chagua wengine, Mkurugenzi atalipitisha na kuendelea na kazi” amesema Mnyeti
Aidha amewataka wachaguliwe watu ambao ni waadilifu na wenye uweledi na kufanya kazi kwa ufanisi na kuwa na hofu ya Mungu ili waingie kwenye mabaraza mabaraza hayo.
Pia amesema anataka watendaji wote watakaochaguliwa wafanyiwe uchunguzi na vyombo husika ili kubaini kama watafaa kufanya kazi katika baraza hilo.
Moja ya mkazi wa kata ya Murray amelililamikia baraza hilo kwa kuchukua rushwa kwa wananchi, pia amewataka wananchi kupata elimu juu ya sheria.