Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma amejiuzulu mara baada ya shinikizo kubwa kutoka ndani ya chama chake kumtaka aachie ngazi.
Kupitia hotuba yake aliyoitoa na kurushwa moja kwa moja na televisheni, Zuma amesema kuwa anajiuzulu mara moja ingawa hakubaliani na uamuzi wa chama cha ANC.
Aidha, Zuma mwenye umri wa miaka 75 amekuwa akikabiliwa na shinikizo kubwa kutoka ndani ya chama chake la kumtaka ampe nafasi makamu wake wa Rais, Cyril Ramaphosa, ambaye kwasasa ndiye kiongozi mpya wa chama hicho.
“Hakuna maisha yatakayopotea kwa sababu yangu wala ANC haiwezi kugawanyika kwa sababu yangu. Kwa hivyo nimefikia uamuzi wa kujiuzulu kama rais wa nchi mara moja, licha ya kutokubaliana na uamuzi wa chama changu, siku zote nimekuwa mwanachama mwenye nidhamu wa ANC, Ninapoondoka, naahidi nitaendelea kuwatumikia watu wa Afrika Kusini sawa na ANC, chama ambacho nimekitumikia maisha yangu yote,”amesema Zuma
-
Zuma atakiwa kuchagua moja ‘mbivu ama mbichi’
-
ANC yaahirisha kumjadili Zuma
-
Netanyahu aingia matatani, wapinzani wamtaka ajiuzulu