Madiwani wa Halmashauri ya Buchosa wilayani Sengerema wamemuomba Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa aondoke na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Cyprian Luanda baada ya kutoridhishwa na utendaji kazi wake.

Wametoa ombi hilo katika kikao cha Waziri Mkuu na watumishi Halmashauri ya Buchosa akiwa katika siku ya kwanza ya ziara yake ya kikazi mkoani Mwanza.

Aidha, Majaliwa amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella kwenda katika halmashauri hiyo na kufanya kikao cha pamoja kati ya Madiwani, Mkurugenzi na watumishi ili kubaini changamoto zilizopo na kuzitafutia ufumbuzi.

Katika hatua nyingine, Majaliwa ameweka jiwe la msingi katika hospitali ya Halmashauri ya Buchosa wilayani Sengerema, ambapo ujenzi wake hadi kukamilika unatarajiwa kugharimu sh. bilioni 10.55.

Hata hivyo, Majaliwa amezindua madarasa manne ya Kidato cha Tano na Sita katika Shule ya Secondari ya Nyehunge wilayani Sengerema na kuwataka wanafunzi wasome kwa bidii.

 

Video: Chadema wavamia tume ya uchaguzi, Fuvu ofisi ya mawakili lazua taharuki
Magazeti ya ndani na nje ya Tanzania leo Februari 16, 2018