Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 16 Februari 2018, atawaapisha Mabalozi wawili aliowateua kuiwakilisha Tanzania katika nchi za Nigeria na Sweden.

Akitoa taarifa hiyo Katibu Kiongozi, Balozi John Kijazi amesma kuwa mabalozi hao watakaoapishwa ni Muhidin Ally Mboweto ambaye ameteuliwa kuwa wa Tanzanaia nchini Nigeria na Dkt. Willbrod Peter Slaa ambaye ameteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Sweden.

Uteuzi wa Mabalozi hao kuiwakilisha Tanzania katika nchi walizopangiwa umeanza jana tarehe 15, Febtuari 2018.

Rais Magufuli alimteua Dkt. Slaa kuwa balozi November, 23, 2017 taarifa ambayo ilitolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU, Gerson Msigwa.

Mtoto arudishwa nchini baada ya wazazi kuhukumiwa kunyongwa
Video: Chadema wavamia tume ya uchaguzi, Fuvu ofisi ya mawakili lazua taharuki