Tegolena Uiso ambaye ni dada wa marehemu, Akwilina Akwiline ambaye ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), aliyeuawa kwa kupigwa risasi, amesema hawatapokea mwili wa marehemu huyo bila kuelezwa nini kilichomuua ndugu yao.

Tegolena amesema hayo baada ya kuambiwa kuwa mochwari ya Muhimbili hutoa ripoti ya uchunguzi baada ya siku 14.

Aidha kama dada wa familia na wanandugu wengine wamekubaliana kuwa ni vyema wakapewa ripoti kuhusu kilichogundulika na kumsababishia kifo ndugu yao.

”Sisi tumekuja kwa ajili ya kujua hasa ndugu yetu nini kimemkuta hatuwezi kupokea mwili bila ripoti wanatuambia ni baada ya wiki mbili sina hakika kama watakuwa hawajabaini kitu chochote, hatuwezi kuuchukua mwili mpaka tupewe sababu” amesema dada wa marehemu.

Amesema mpaka sasa wamezungumza na Mkuu wa Chuo cha Usafirishaji NIT, Profesa Zakaria Mhanilwa ambaye bado anawasiliana na madaktari na hawajajua iwapo atakuja na majibu sahihi.

 

Eden Hazard aiweka njiapanda Chelsea
Safari ya Mavugo yanukia Msimbazi