Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani FIFA limeongeza tiketi kwa Tanzania kwaajili ya fainali za kombe la Dunia zitakazochezwa Russia mwaka huu.

Kwa shabiki yeyote anayetaka kwenda kushuhudia fainali hizo za Kombe la Dunia awasiliane na idara ya mashindano ya TFF kwa utaratibu wa namna ya kupata tiketi hizo.

Ngwe hii ya pili ya tiketi za Kombe la Dunia imefunguliwa Februari 15, 2018 na itafungwa Machi 12, 2018.

Ikumbukwe awali FIFA walitoa tiketi 290 kwa Tanzania ili kushuhudia fainali hizo za Kombe la Dunia kabla ya zoezi hilo kufungwa mwezi Januari na sasa imefunguliwa ngwe nyingine ya tiketi hizo.

Sumaye aitaka serikali kuchukua hatua za haraka
Video: Waziri Dkt. Kigwangalla awajibu Polisi