Padri Patrick Henry Edet, amekiuka miiko ya kanisa katoliki la Roma, baada ya kutangaza kuwa mwili wake umeshindwa kupambana na nguvu za nafsi yake na anatimiza andiko la kuzaliana na kuongeza dunia hivyo ameamua kuoa.
Padri huyo ambaye mwaka jana Novemba alitengwa na kanisa la Roma jimboni kwake Uyo, nchini Nigeria akidai kuwa haoni umuhimu wa kuumiza nafsi yake kwa kile anachoamini kuwa kuoa si dhambi bali ni utamaduni tu wa kikatoliki ambao amesema hauna maana kwa sasa.
Padri huyo tayari ameshahudumia kanisa katoliki kwa miaka 11 amesema kuwa kanisa liangalie upande wa pili wa sheria hiyo kwani kuna matatizo mengi yanatokea kutokana na sheria hiyo ya kutokuoa au kuolewa kwa watumishi wake.
Amesema ”Kuanzia leo, naachana na masharti magumu ya kanisa katoliki, mwili wangu umeshindwa na nguvu ya nafsi. Mtanisamehe wale wote waumini ambao nimewaudhi kwa maamuzi yangu, mimi nitimize andiko lake la kuzaliana dunia. Ninataka kuwa mtu huru wa mwili na nafsi na kwa andiko hilo natangaza rasmi kuwa mwezi Machi 17 mwaka huu nafunga ndoa hivyo basi nitakuwa muumini wa kawaida” Amesema Fr. Henry.
-
Ukaguzi wa magari binafsi kuanza rasmi machi
-
Injili ya mchungaji yamtia mbaroni, ”…Wanawake chanzo cha matatizo duniani’’
-
Fahamu nguvu ya ndoto katika mahusiano yaliyovunjika
Papa Fransis, ambaye ni kiongozi mkuu wa kanisa katoliki duniani alipotembelea baadhi ya makanisa nchini Kenya na Nigeria wakimtaka aiangazie nchi hiyo ikiwemo kufikiria namna ya kuboresha baadhi ya masharti magumu ya viongozi wa dhehebu hilo ikiwemo kuoa.