Mbunge wa jimbo la Kigoma Mjini, Zitto Kabwe amefunguka kuwa kitendo cha yeye kukamatwa na kulazwa ndani kwa usiku mmoja kumemfanya agundue kuwa kuna Watanzania wengi wanateseka na kupata shida kwenye vituo vya polisi nchini.
Ziito amesema kuna uvunjifu mkubwa wa sheria unaofanywa na Jeshi la polisi ambao hauvumiliki,
amesema sheria inataka mtuhumiwa akae ndani kwa masaa 48 kisha polisi awe ameshamfikisha mahakamani hali ambayo ni tofauti.
”Tumekutana na watu wamekaa ndani siku 3 hata maelezo tu hawajaandika, wengine wana siku 20 wapo ndani hawajafikishwa mahakamani” amesema Zitto Kabwe.
Aidha Zitto ameelezea jinsi alivyoshuhudia kijana mmoja aliteswa mpaka kuvunjika mbavu na amekaa zaidi ya siku saba bila kufikishwa hospitali kwa ajaili ya matibabu.
-
Tamko la Zitto baada ya kutoka selo
-
Zitto ang’ang’aniwa selo, anyimwa dhamana
-
Zitto aachiwa huru kwa dhamana ya mamilioni
”Mpaka jana tunaondoka hajapelekwa hospitali, tulipozungumza na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro tulimweleza hilo, kuna watu ni wagonjwa hawajapelekwa hospitali akasema atashughulikia sasa sijui kama yeye alikuwa hajui hilo” amesema Zitto.
Mbali na hilo Zitto Kabwe amesema hali kiujumla ya nchi yetu kwa sasa ni tata kwa kuwa suala la mauaji yameendelea kutokea kinyume na mazoea yaliyokuwepo kipindi cha nyuma na kudai kuwa kuna kila sababu ya uchunguzi wa mauaji hayo kuanzia yale ya Kibiti mpaka haya ambayo yanaendelea sasa kuchunguzwa na vyombo huru na si jeshi la polisi kwa kuwa jeshi hilo nalo linatuhumiwa.
Zitto Kabwe amesema hayo jana Februari 23, 2018 akiongea na waandishi wa habari.