Maelfu ya waandamanaji wamefurika katika mitaa ya jiji la Tel Aviv nchini Israel wakipinga uamuzi wa nchi hiyo kuwafukuza wahamiaji zaidi ya 20,000 wanaotoka Afrika.
Maandamano hayo yaliyofanyika jana yaliibua kundi lingine la waandamanaji waliokuwa na idadi ndogo wanaounga mkono uamuzi wa Serikali ya nchi hiyo dhidi ya wahamiaji kutoka Afrika.
Mapema Februari mwaka huu, Israel iliwataka wahamiaji 20,000 kutoka Afrika kuondoka nchini humo vinginevyo wangefungwa jela.
- Magazeti ya ndani na nje ya Tanzania leo Februari 25, 2018
- Marekani kuyawekea vikwazo mataifa yanayoshirikiana na Korea Kaskazini
“Leo tunaandamana kupinga sheria ya Serikali ya Israel ya kuwafukuza raia wa Eritrea au Sudan au wakimbizi wa aina yoyote kwenda kwenye nchi nyingine. Huo sio mfumo wa kweli kwamba unamuondoa mtu ili akauawe kwenye nchi nyingine,” alisema mmoja wawaandamaji aliyejitambulisha kwa jina la Braham Nagasi.
Waziri Mkuu wa Israel, Benjamini Netanyahu alisema kuwa serikali yake inatoa $3,500 na tiketi ya ndege kwa kila mhamiaji anayerejea Sudan au Eritrea na kwamba kwa watakaokataa mpango huo watakabiliwa na kifungo.