Chama cha Jubilee nchini Kenya kimesema kuwa mkopo wa mabilioni ya shilingi ambao serikali imechukua ulikuwa tayari umeingizwa katika bajeti ya mwaka 2017/2018 na waziri wa fedha.
Hayo yamesemwa na Makamu wa Rais wa Nchi hiyo, William Ruto baada ya baadhi ya Wakenya na viongozi kukosoa hatua hiyo ya serikali ya kuamua kukopa shilingi bilioni 200 kutoka katika taasisi za fedha za kimataifa.
Ruto amesema kuwa serikali ya Kenya imechukua mkopo huo kwa sababu imejipanga hivyo wananchi na viongozi hawapaswi kuwa na hofu kwa sababu itausimamia vizuri katika matumizi yake.
Hata hivyo, Mbunge wa Jimbo la Garissa Mjini Aden Duale ameungana na makamu huyo wa rais kwa kusema kuwa Kenya inauwezo wa kulipa deni hilo ukikilinganisha na pato la ndani la taifa (GDP) ambalo hivi sasa limefikia asilimia 56.