Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Mbunge wa Jimbo la Hai, Freeman Mbowe amelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC ya Moshi Kilimanjaro.
Mkurugenzi wa Itikadi, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa CHADEMA, John Mrema amethibitisha juu ya taarifa hiyo na kusema kuwa Mbowe amelazwa toka jana Machi 4, 2018 na mpaka sasa anaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali hiyo.
“Ni kweli Mbowe amelazwa toka jana yupo pale KCMC na anaendelea kupatiwa matibabu, siwezi kuzungumzia kinachomsumbua kwa kuwa ugonjwa ni siri ya mgonjwa na daktari, hivyo tutambue tu anaumwa amelazwa KCMC” amesema Mrema.
-
Nape: Huu ni ushetani wa baadhi ya viongozi wa Afrika
-
Video: Askofu Kakobe afunguka tena, Msajili aitisha tena Chadema
Mbowe siku za karibuni amekuwa na mizunguko mingi mno kuanzia kwenye kampeni za uchaguzi wa Kinondoni na Siha lakini pia safari za Mbeya mara kadhaa kwenye kesi ya Mbunge wa Mbeya Mjini na Katibu wa CHADEMA Nyanda za Juu Kusini.